site search by freefind advanced

UONGOZI WA HUDUMA

Huduma hii ina uongozi wake ambao unahusisha viongozi Wakuu wa idara mbalimbali na viongozi wa mitaa. Kiongozi mkuu wa huduma hii ni ndugu Johannes Kasimbazi ambaye anashirikiana na timu ya, endelea

HUDUMA ZILIZO CHINI YA RHEMA OUTREACH:

SOMA NENO LA MUNGU HAPA

Mafundisho ya neno la Mungu

Maombi kwa mwenye pepo

TUMEITWA KUMTUMIKIA YESU

UTAMBULISHO

Je laweza neno jema kutokea Nazareti? Kama vile Nazareth ulivyokuwa machoni pa wayahudi wengi mji uliodharaulika; Bukoba pia umekuwa mji duni machoni pa wengi. Hii ni kutokana na mfululizo wa majanga kama ukimwi uliojitokeza kwa mara ya kwanza Tanzania katika mji huu mwaka 1983, historia mbaya ya ugonjwa wa Syphilis, wakina mama waliosambaa Afrika mashariki miaka ya 60 katika biashara ya umalaya, vita ya Idd Amini 1978, ajali mbaya ya meli 1996 na mengine mengi. Hata hivyo wengi wasilojua ni historia ya uamsho uliopita kama mafuriko miaka ya ’30 kwa zaidi ya miaka 50. Uamsho huu ulioitwa uamsho wa Utakatifu kwa vile ulivyosisitiza juu ya toba na kutengeneza maisha na kutembea katika nuru ulianzia Rwanda wakati watu wawili waliokuwa wanasali pamoja lakini wakiwa na uhasama kati yao walipokutana ghafla sehemu waliyokuwa hawategemei na ikawa vigumu kwao kukwepana. Ndipo Roho Mtakatifu alipowabana na badala ya kugombana waliangukiana na kutubu kila mtu kwa mwenzake. Waliosikia habari ya maadui hawa walielewana kwa muujiza ndipo nao waliguswa na Mungu na kuanza kutubu dhambi zao waliofanya hata kama walikuwa makanisani. Uamsho huu ulipitia Uganda na kuingia katika mkoa wa Kagera. Upendo wa kweli kati ya ndugu ulikuwa ni tabia ya uamsho huu. Ndipo shetani alinyanyuka kujaribu kufuta kabisa baraka za uamsho huu kwa udini, uharibifu na majanga. Lakini habari njema ni hii "Karama za Mungu hazina majuto....." endelea Wana UCF wakisikiliza neno la Mungu

HUDUMA

Huduma hii kama huduma nyingine yoyote isiyo ya kibiashara inafanyika kwa kutegemea michango na sadaka. Ni jambo la muhimu ujue kuwa injili, inahubiriwa kwa kujitoa kwa watu katika kuipeleka na mhusika ni wewe. Maana neno la Mungu katika kitabu Warumi 10:14-15 lasema "..... Tena wamwaminije yeye wasiye msikia?Tena wahubirije, wasipo pelekwa?......." Hivyo Ili tuweze kuufikia mji wa Bukoba, Mkoa mzima wa Kagera,na Tanzania yote, mchango wako ni wa muhimu kwetu na kila ukichangia elewa umewekeza katika ufalme wa Mungu na umejiwekea akiba mbinguni. Na si hilo tu bali wewe pia umehusika kuhubiri injili kwa kujitoa kwako.Changia huduma hii kwa kujaza fomu hii hapa au kwa kuweka katika akaunti ya huduma: RHEMA OUTREACH MINISTRIES. "NBC TAWI LA BUKOBA" AKAUNTI NAMBA 027201138819. Na kwa wale walio nje ya Tanzania watumie Swift Code hii hapa NLCBTZTX NLCBTZTO wakati wa kutuma michango yao.