MAFUNDISHO

Moja ya mambo ambayo ni muhimu kwa Bwana Yesu ni kuona mafundisho yakitolewa kwa watu wake. Ni kwa sababu hii tunaona toka mwanzo akisisitiza jambo hili siku anapaa mbinguni katika Mathayo 28:20 "na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi; na tazama.......'.

Kabla ya kupaa kwake mbinguni tunaona katika Yohana 21:17 Yesu anaagiza "....lisha kondoo wangu".

Katika Yohana 4:34 tunaona dhahili kwamba kuyafanya mapenzi ya Mungu ndio chakula. Yohana 6:27 inasisitiza jambo hilo hilo tena kiasi kwamba tunaona wazi kuwa kufundisha ndiyo mapenzi ya Mungu.

Huduma hii inahitaji kuona wanafunzi wa Bwana Yesu wanapata chakula cha kutosha kupitia mafundisho ya Bwana Yesu. sisi katika huduma tunahitaji kuwa waaminifu katika huduma hii maana Bwana wetu Yesu katika Matayo 24:45 anasema; "Ni nani tena aliye mtumwa mwaminifu na mwenye busara? Bwana atamuweka mtu huyo katika nafasi ya kusimamia kuwapa watumishi wengine chakula katika wakati muafaka." (Tafsiri hii ni kutoka katika Biblia ya NENO.)hivyo basi katika huduma hii Bwana katupatia nafasi ya kuwapa na watumishi wengine mafundisho ili wakue kiroho, pia wapate kuwa watumishi waaminifu. Kumbuka katika maneno hayo Yesu anasema mtumishi mmoja anapewa usimamizi wa kuwapa watumishi wengine mafundisho katika wakati ambao chakula hicho kitakiwapo; katika Luka 12:42 anamuita msimamizi huyu wakili au meneja; na siku zote katika Rhema Outreach Ministries kuna mafundisho katika wakati muafaka toka kwa viongozi waaminifu walio kabidhiwa na Bwana kulipatia kundi lake kama Bwana anavyotoa. Yohana 10:9 tunaona wazi kila aliyeingia kwenye zizi la Bwana Yesu atapata malisho. Karibu katika zizi hili la Bwana upate malisho.

Bonyeza hapa chini kupata masomo mbalimbali; kula na ushibe:

1.ufalme wa Mungu

2.Ufalme wa Mungu-somo la 2

3.MUNGU ANATAKA KUPONYA UGONJWA WAKO LEO.

4.MAPAMBAZUKO

5.MAPAMBAZUKO #2

6.MAPAMBAZUKO #3

7.MAPAMBAZUKO #4

8.MAPAMBAZUKO #5

9..Kiwango cha Mungu

10..Kukubali mwaka 2010 na wimbo

11..Kuona nyuma ya mlima

12..Mtu aliyeokoka ni wa thamani mbele za Mungu

13..Ubatizo wa Roho mtakatifu na Moto

14..Kiwango cha Mungu-Double agent

15..Yesu alidhihirishwa ili azivunje kazi za shetani

16..Kushindania imani

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU