"MAOMBI"

Kuomba ni msingi mkuu wa huduma hii ya Rhema Outreach Ministries na kwa sababu hiyo hiki ni kipaumbele cha kila huduma tuifanyayo. Kuna timu au idara ya maombezi ambayo hujishughulisha na habari za maombezi mbalimbali na kuiombea huduma. Tena kuna maombi ambayo watu wote katika fellowship upewa na kutakiwa kufunga na kuomba. Haya tunayaita maombi ya mnyororo, kwani kila mtaa upewa siku moja katika wiki ya kufunga na kuomba maombi hayo na hivyo tunajikuta tunaomba maombi hayo kila siku ya wiki. Na kila mmoja anatakiwa kuwa mwaminifu katika kufunga na kuomba. Mambo ya kuombea katika maombi ya mnyororo ubadirika kila mara kama Roho anavyotuongoza na siku za mitaa kuomba ubadirika mara moja kwa mwezi.

Jambo muhimu ni kwamba katika maombi ya mnyororo kuna jambo la kuombea kila siku, kuanzia nchi hadi kanisa. Na pia kuna maombi ya Viongozi wa fellowship ambayo ufanyika mara kwa mara kwa ajili ya kuiombea huduma.

Na kuna maombi ya Wana fellowship wote ambayo ufanyika mara moja kwa mwezi.

Kuna mkesha wa wanafellowship wote ambao ufanyika mara moja kwa mwezi na mkesha huu ufanyika katika mojawapo ya kanisa lolote linalokubali kutupa nafasi hiyo ya kufanyia mkesha. Kuna maombi na mkesha mahususi kwa ajili ya huduma kama Kwaya ya Unity Christian Fellowship ambapo wana Kwaya upanga kufunga, kukesha na kuombea huduma yao ya Kwaya. Tena kuna mikesha ya mitaa ambapo wana fellowship uomba katika mitaa yao kila wiki mara moja.

kwa mfano mtaa wa Migera ufanya mkesha kila jumatatu ya wiki, mtaa wa magoti ufanya mkesha kila jumatano ya wiki na mtaa wa National housing ufanya mkesha kila ijumaa ya wiki n.k. Na kila mtaa ufanya mkesha huko huko mtaani kwao katika nyumba waliyochagua wana mtaa wenyewe.

Kuna maombi ya kuombea huduma mbalimbali zinazokuwa mbele yetu katika nyakati mbalimbali, kama mikutano ya injili, au semina ambazo zinakuwa zimetayarishwa. Maombi haya ufanywa na wana fellowship wote chini ya uongozi wake.

Kuna maombi ya shule ya uponyaji, huduma ambayo ufanya maombi maalum kwa ajili ya watu wote walio katika mateso ya magonjwa na udhaifu mbalimbali wa mwili.

Mara kwa mara kuna maombi maalum kuombea watu walio na shida mbalimbali ambao uzileta kwa viongozi ili wapate kuombewa. Kufunga na kuomba bado ni kipaumbele cha huduma, ungana nasi katika kuombea huduma hii na kuliombea kanisa. Ungana nasi kuuombea mji wa Bukoba upate kubadilika na kurudi kwa Bwana. Tusaidiane kuuombea Wokovu kwa mji wa Bukoba na kuivunja Roho ya Dini na udhehebu iliyotawala eneo hili!.

Fuatilia maombi ya kuombea pamoja nasi kila mara hapa

Fuatilia Ratiba hii ya maombi na kuomba pamoja nasi mwaka mzima hapa

Fuatilia Ratiba ya huduma mbalimbali hapa

Je una jambo unahitaji maombi? Ebu andika hapa chini na kuyatuma kwetu ili tusaidiane kuomba. Kumbuka kututumia ushuhuda wa nini Mungu amekufanyia baada ya maombi haya kwa kuandika barua kwa anuani iliyo katika ukurasa wa kwanza wa tovuti hii, au kutuandikia kwa email rhematz@rhematanzania.org au hata kwa kupiga simu namba +255 713 095 111 na +255 768 325 841.

MSIJISUBUE KWA NENO LOLOTE; BALI KATIKA KILA NENO KWA KUSALI NA KUOMBA, PAMOJA NA KUSHUKURU, HAJA ZENU NA ZIJULIKANE NA MUNGU. FILIPI 4:6

 

UNA MAOMBI? ANGALIA HAPA

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU