"MAOMBI TUNAYOOMBA SASA"

TAREHE   MAOMBI YA KUOMBA VIPENGELE KATIKA MAOMBI
05.07.2010 1. Ombea kanisa la Bukoba Yeremia 9:1
  a) Tubia matengano katika kanisa la Bukoba 1 Yohana 1:8-10
  b) Ombea umoja wa kweli katika kanisa la Bukoba Yohana 17:21
  c) Vunja roho ya kuigiza(usanii) katika ukristo  
  d) Liombee kanisa la Bukoba kuishi kwa imani Waebrania 10:38
       
  2. Ombea taifa Isaya 55:6
  a) Ruhusu roho ya kufitinika kwa wapinga Kristo kwa mipango yote waliyonayo juu ya ukristo na wakristo Tanzania. Matayo 12:25
  b) Omba kila hila waliyonayo wapinga Kristo na wakristo iwapate wao Daniel 6:25; Esta 7:10
  c) Endelea kuomba mkono wa Bwana kuwa mzito kwa watu wote wanaomsaliti Yesu kwa ajili ya pesa.  
  d) Ombea wagombea wakristo katika nafasi mbalimbali ushindi juu ya vikwazo mbalimbali na kukubarika mbele za watu wote  
       
  3. Ombea kongamano la maombi la kitaifa Dodoma  
  a) Maandalizi yote ya watu na ya huduma yenyewe yafanikiwe  
  b) Vunja kila upinzani wa kipepo na kibinadamu juu ya kongamano hilo.  
       
23.08.2010 1a) Jiombee binafsi hamu/shauku yako iwe ni katika kumjua Mungu. Yeremia 9:24; Mathayo 7:9
  b) Jiombee binafsi pamoja na Unity Christian fellowship uaminifu katika wito wetu wa Kuomba. Habakuki 2:1a
  c) Ombea ndugu na dada katika mtaa wako. Yakobo 5:16
       
  2. OMBEA MJI WA BUKOBA Ezekieli 22:30
  a) Uombee mji wa Bukoba roho ya toba na maombolezo tokana na maovu yake yote. Yona 3:4-9
  b) Omba Mungu alitume neno la kuuponya Zaburi 107:19-20;
  c) Omba neema ya wokovu iwafikilie watu wote. 2 Petro 3:9;Luka 19:10
       
  3. OMBEA UCHAGUZI  
  a) Ombea amani ya Bwana itawale kila eneo Zaburi 115:3
  b) Omba makusudi yote ya waovu yasifanikiwe Zaburi 9:16-20
  c) Omba Mungu atulinde na hila za wapinga Kristo na mipango yao isifanikiwe. Endelea kukiri Zaburi 83:1-18  
       
01.10.2010 1. Kuombea nchi  
  a. Tubu kwa ajili ya maovu na dhambi zilizofanywa na kanisa katika nchi hii, na hata zile zinazohusiana na mambo ya uchaguzi. Mfano kuwatuminia wanadamu kuliko Mungu, tamaa ya vitu na heshima toka kwa watawala, kutojali nafasi yake na hatima ya nchi Mungu aliyoweka mikononi mwetu n.k. Nehemia 1:6-9, Daniel 9:4-10
       
  b. Ombea kanisa kusimama imara kupingana na makusudi yote mabaya ya shetani juu ya taifa la Tanzania katika uchaguzi. Kanisa likatae suluhu yoyote na shetani pamoja na mawakala wake. 2 Wafalme 21:1-7; 2 Nyakati 20:2,
       
  2. Ombea hali ya kisiasa  kabla na baada ya uchaguzi.  
  a. Kuvunja hila na mipango ya kishetani inayoandaliwa kwa ajili ya kuiba kura, kuvuruga uchaguzi, hila, vitisho na machafuko yakiwemo umwagaji wa damu. Mwanzo 11:2-6
       
  3.
  1. Chafua usemi na maelewano katika kambi ya wote wenye lengo baya kwa wakristo na hatima ya ukristo  katika taifa la Tanzania kupitia mgongo wa siasa na uchaguzi wa 2010.
1 Samwel 13:14, 18:8,9,22:1
       
  4. Ombea wagombea walioletwa na Mungu kwa ukombozi kata, majimbo na taifa la Tanzania.  
  a. Ulinzi wa Mungu  
  b. Kutambulikana kwa wananchi.  
  c.
  1. Msaada wa Mungu.
 
       
   

Kuombea UCF

Hesabu 13:30 ;Ayubu  19:2
  5.
  1. Ombea ubadilishaji wa jina la viwanja vyetu, pia kuongeza viwanja vingine Mungu atutetee.
1Yoh 5:14
       
  6.a.
  1. Mshukuru Mungu kwa jinsi alivyotusaidia tangu mwanzo wa mwaka 2010. Shule ya uponyaji,arusi n,k
Zaburi 124:1,3
  b. Ombea ratiba iliyobaki ya UCF, semina, mkutano wa injili na maombi ya kanisa, shule ya uponyaji, arusi  na mikutano ya viongozi  
       
  7.
  1. Ombea uanzishaji wa redio Mungu atufanikishe kupata eneo, leseni, vifaa k.m transmitter, antenna; studio watangazaji na mafundi.
 
       
  8a.
  1. Omba Mungu akufungulie karama za Roho Mtakatifu katika maisha yako binafsi.
1 Wakorintho 14:1, 12.
  b. Ombea kanisa la Unity Christian Fellowship kudhihirisha karama za Roho Mtakatifu katika huduma yetu.  
       
2.12.2010 1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya shule ya uponyaji, mafundisho na nguvu zake za kuponya. Zaburi 107:19-20; 103:1-4; Isaya 42:8
  b. Ombea wote walioponywa kuendelea kutunza uponyaji wao kwa kung'ang'ania neno la Mungu. Mithali 4:20-22
  c. Ombea waliookolewa kuendelea mbele katika Bwana. Wagalatia 4:19
  d. Endelea kuombea watu wenye shida mbalimbali neema ya kupeleka shida zao kwa Matayo 14:13-14
    Yesu.  
     
  2. Endelea kuliombea kanisa la Tanzania mzigo wa kuomba kwa ajili ya taifa. Yeremia 9:1
  b. Endelea kuombea nchi yetu ya Tanzania amani. Yeremia 29:7,11
  c. Omba Mungu azidi kuliatamia taifa hili la Tanzania kwa kila jambo. Zaburi 74:2, 29
       
06.12.2010 1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya wema na fadhili zake nyingi binafsi, familia, taifa, huduma n.k. Zaburi 107:8
  2. Ombea maombi maalum yatakayofanyika tarehe 10-11/12/2010 kwa ajili ya taifa letu. Zaburi 37:5
  3.a Jiombee binafsi na UCF kutokutulia katika maombi kwa ajili ya Tanzania. Isaya 62:1,6-7
  b. Funga roho ya kutangatanga katika ulimwengu wa roho.  
  c. Omba Mungu akufundishe/ atufundishe vita (roho ya kupambana mpaka mwisho) Zaburi 18:32-34
  4. Endelea kuombea ulinzi na amani ya Mungu juu ya taifa letu usiku na mchana. Yeremia 29:9
       

Maombi hayo hapo juu ni ya kuliombea kanisa ( yaani watu wote waliookoka) katika mji wa Bukoba, Kagera na Tanzania kwa ujumla wake. Ebu husika katika kufunga na kuomba kwa ajili ya mwili wa Kristo.

Page 1|2|3

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU