"MAOMBI TUNAYOOMBA SASA"

TAREHE   MAOMBI YA KUOMBA VIPENGELE KATIKA MAOMBI
10.06.2012 1a). Mshukuru Mungu kwa uponyaji wa watu wake waliopokea uzima, waliopokea watoto kwa imani, waliopokea wokovu, waliowekwa huru mbali na mateso, waliowekwa huru mbali na mateso, na waliowekwa huru dhidi ya dhiki mbalimbali. Zaburi 118
  b).
  1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya neno lake alilotuma kuponya, kufungua, kuokoa, kuweka huru na endelea kushukuru kwa ajili ya jina la Yesu lenye nguvu na damu ya Yesu inenayo mema.
Zaburi 107:19-20 Yohana 14:13-14
  c) Mshukuru Mungu kwa ajili ya kanisa (UCF) kulitumikia kusudi la Mungu. Matendo 13:3-6
  d) Kataa kubeba utukufu wa Mungu na kubali kumpa Mungu utukufu katika idara zote. Matendo 14:15
  e) Kataa roho ya kujiinua, na hitaji unyenyekevu 1Petro 5:5(b)-6
  f) Ficha uhai wa UCF ndani ya damu ya Yesu, na kataa roho ya malipizi kwa wote waliotumika. Wakolosai 3:3
       
  2a). Endelea kuomba Mungu akupe kiwango kingine cha utumishi katika shule nyingine za uponyaji zijazo. Warumi 1:17 2Wakorintho 3:18
  b.) Endelea kuombea wachanga na wote walioguswa katika uponyaji, Mungu akamilishe uzima ndani yao kiroho na kimwili Wagalatia 4:19
  c.) Endelea kukabidhi maisha yako, huduma, familia, kanisa, taifa kwa Bwana katika mwaka 2011 na kumsihi akuongoze katika makusudi yake yote. Zaburi 37:5
       
  3. Ombea nchi yetu Tanzania, huku ukivunja roho za vurugu za kidini nchini na kuchoma makanisa kwa kisingizio cha muungano. Zaburi 35:1-2
       
  4. Ombea semina ya tarehe 02/07/2012 hadi 05/07/2012 huku ukiombea mahitaji yote.  
       
       
       
       
       
       
       
       

Maombi hayo hapo juu ni ya kuliombea kanisa ( yaani watu wote waliookoka) katika mji wa Bukoba, Kagera na Tanzania kwa ujumla wake. Ebu husika katika kufunga na kuomba kwa ajili ya mwili wa Kristo.

Page 1| 2|3

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU