SHUHUDA

"Wakushangilie, wakufurahie, wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe BWANA. Zaburi 40:16

Ushuhuda ni kile kitendo cha kumshukuru na kumuabudu Mungu kwa matendo yake makubwa aliyoyafanya kwako au kwa watu wengine kwa kuwaonyesha ushahidi wa jinsi Mungu alivyokuwa muaminifu kwako au kwa jamaa yako au kwa mtu mwingine yeyote.

Ushuhuda hujenga na kuiimarisha imani yako.

Jambo hili ni zuri na linawatia moyo wengine lakini pia linamuaibisha Shetani na zaidi ya yote linamtukuza Mungu wetu ambaye siku zote amekuwa akifanya mambo makubwa ya ajabu hata kuzidi ufahamu wetu.

Ushuhuda ni msaada hata kwa watu wengine maana kwa kumuongezea imani mtu mwingine unaweza kumletea mtu huyo muujiza huo huo.

Ushuhuda umfanya Mungu wetu ainuliwe katika kiti cha enzi na kuabudiwa.

Ushuhuda ni jambo la muhimu kwa kila mtu na usiache kushuhudia watu wengine yale Mungu anayoyafanya katika maisha yako.

Ebu soma Shuhuda za watu hawa uone yale Mungu anafanya katika maisha ya watu wengine:

Maisha yangu ya ndoa

Mateso yangu yalikwisha nilipookoka

Nimeponywa shida ya pepo

Nilidharau wokovu na sasa nimeokoka na Mungu kaniponya

Yesu ndio chanzo cha badiliko langu

Ushuhuda wa wanafunzi wa Bukoba Sekondari 2000-2001

Je wewe nawe una Ushuhuda? Kuna jambo unataka kumshukuru Mungu kwa kulifanya katika maisha yako na linaweza kuwasaidia na wengine? je unataka tuungane nawe na kumshukuru Mungu kwa yale anayoyafanya katika maisha yako, familia yako, jirani yako, mtoto wako wa kiroho, ndugu yako, mfanyakazi mwenzio, mwanafunzi mwenzio, n.k.? Tutumie ushuhuda wako kwa kutuandikia kupitia email hii: rhematz@rhematanzania.org na kwa mawasiliano zaidi bonyeza hapa.

 

 

 

 

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU