USHUHUDA ALIOUTOA NDUGU SALMON KASHAGA:

Nilipokuwa kijana na baada ya kuoa maisha yangu ya ndoa yalikuwa magumu sana kiasi kwamba nilidhani mimi na mke wangu hatupendani hata kidogo na labda siku moja tungeweza kuachana.

Lakini baada ya kuokoka kwa kweli nimeona Mungu akinipigania na Mungu akiniongoza katika maisha ya ndoa kiasi kwamba ninapo muangalia mke wangu sasa namuona kama bado ni kijana maana Mungu katutendea mambo mengi makubwa na ya ajabu sana. Ingawa tuna miaka 21 tangu tumeoana kwa kweli naona kama tuna mwaka mmoja tu.

Na hili linanifanya nipende kumshukuru Mungu na kuendelea kumpenda.

Na kwa kweli nitaendelea kupenda mpaka pale atakapokuwa ameniita.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU