SHULE YA UPONYAJI

Tulipokuwa tukimwomba Mungu kuhusiana na watu wake wanaoteswa na magonjwa wakati mwingine wakiwa wanampenda, Mungu alituelekeza kuanza shule ya uponyaji.

Mungu alituongoza kusoma Marko 6:5-6 Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya. Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya pale karibu akiwafundisha watu. ambako Biblia inasema Yesu hakuweza kufanya miujiza mahali ambapo palitawaliwa na kutoamini. Lakini ili kushinda kikwazo hiki na kuwasaidia waliokuwa na hitaji la kuponywa alianza kampeini ya kufundisha katika vijiji vyao ili kuwaondolea kutokuamini kwao.

Wako watu wengi wanashindwa kupokea miujiza yao kwa sababu ya ufahamu mdogo kuhusina na uponyaji wa Mungu. Wengine wameponywa na kupoteza uponyaji baada ya muda mfupi kwa sababu hawakujua namna ya kuutunza uponyaji wao. Aidha wengi hawajui kuwa mara nyingi shetani huleta shambulio la pili (counter attack) mara anapoona mtu ameponywa ugonjwa wake. Ni kutokana na ulazima huu huduma ya Rhema Outreach Ministy imeanzisha shule maalum za uponyaji zinazotoa mafunzo juu ya namna ya kupokea uponyaji na jinsi ya kuutunza. Karibu tushirikiane katika Baraka hii.

 

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU