MUNGU ANATAKA KUKUPONYA UGONJWA WAKO LEO.

Sababu nne kwa nini Mungu anataka kukuponya.

1. ANAO UWEZO/NGUVU YA KUKUPONYA KABISA UGONJWA WAKO WOTE.

Marko 10:27; Waebrania 11:3; 1Yohana3:8.

2. ANAKUHURUMIA NA KUKUPENDA. HATAKI UTESEKE.

Yesu Kristo alikuja kutuonyesha mapenzi ya Mungu. Isaya 53:10; Yohana 1:18 Kila tendo au neno la Bwana lilikuwa linafunua mapenzi ya Baba yake ambaye ni Mungu. Yesu alitufunulia Mungu alivyo. Tunajua ni mapenzi yake kutuponya. Matendo 10:38; Luka 13:15-17; Zaburi 103:2-3.

3. ALIKWISHA KULIPA GHARAMA YOTE ILI UWE NA AFYA NJEMA.

Yesu alikufa msalabani kugharimia adhabu ya dhambi zetu na alipigwa na kuumizwa katika mwili wake ili kugharimia uponyaji wa miili yetu.

Isaya 53: 4-5; Mathayo 8:16-17; 1Petro 2:24

4. AMETUTUMA (KANISA) KUULETA UPONYAJI KWAKO.

Yesu ametuagiza kuweka mikono na kukuombea kwa kuwa anataka kukuponya.

Marko 16:16-17; Yakobo 5:14-15.

YESU ALIDHIHIRISHWA ILI KUHARIBU KAZI ZA SHETANI.

Kazi za Mungu ni zipi na kazi za shetani ni zipi?

Tangu kale watu walijua kazi za Mungu zina msaada kwa mwanadamu Zaburi 78:4, 12-15,26; 92:4, 13-15.

Yesu alipokuja alikuwa akifanya kazi za Baba yake . Kisa cha uponyaji katika birika Yohana 5: 17, 20, 36; Yohana 10:27. Hivyo tunajua kazi alizotenda Bwana Yesu zilikuwa njema Matendo 10:38.

Kazi za shetani alizokuja kuharibu Bwana Yesu ni zipi? Tukitazama yale aliyofanya Bwana tunagundua kazi za ibilisi ni pamoja na magonjwa. Luka 13:16. Tazama Yohana 10:10.

1. YESU ALICHUKUA MWILI ILI AHARIBU KAZI NA AMHARIBU SHETANI.

Shida zilizokuwa katika mwili wa binadamu hakuna anayeweza kuzimaliza isipokuwa kwa kung’oa chanzo chake. Ndiyo maana ilibidi Yesu atoke mbinguni, akachukua mwili wa kibinadamu ili akamate mhalifu katika maficho yake. Waebrania 2:14.

Dhambi na magonjwa vyote vilitokea kona moja na vinampeleka mwanadamu katika uharibifu. MAUTI!!!

2. DAMU YAKE ILIPOMWAGIKA.

Biblia utufundisha uzima umo katika damu. Walawi 17:11.

Kwa vile shetani ameleta mauti Yesu alimwaga damu pale msalabani ili uzima wa Mungu ufike duniani na kuwafikia wanadamu

Damu ilipomwagika ushindi ulikuja kwako kwani uzima wa Mungu ulimeza mauti. Ufunuo 12:11.

3. MABADILISHANO KALVARI.

Kazi ya ajabu ilifanyika pale Kalvari ni mabadilishano. Yesu akichukua shida zetu na kukabiliana na ugumu wake na kutupatia Baraka zake.

Yesu katika sura ya jenerali aliyeshinda vita. Wakolosai 2:13-15

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU