UBATIZO WA HATARI AU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NA MOTO .

Mathayo 3:5-12 Haya ni maneno ambayo Yohana mbatizaji aliyaeleza juu ya ubatizo wake akimtambulisha yule atakaye kuja nyuma yake. Yohana alisema ya kwamba hata yeye hastahili kufunga gidamu ya viatu nyake yeye, yaani Yesu. Alisema kwamba yeye Yesu atabatiza kwaROHO MTAKATIFU na kwa MOTO.

Ubatizo wa Roho mtakatifu na wa moto ni mambo yanayoenda pamoja. Ni ubatizo unaokwenda sambamba na ubatizo wa Roho mtakatifu. Moto katika Biblia unazungumzia habari ya utakaso.

Mathayo 17:10-13 Biblia inamzungumzuia Yohana mbatizaji ndiye Eliya ajaye. Yeye alikula nzige na asali ya mwituni na vazi lake lilikuwa ni ngozi. Watu waliwafananisha Yohana na Eliya kwa sababu Eliya naye alikuwa anavaa kama Yohana alivyokuwa anavaa.(2 wafalme 1) Hivyo namna ya muonekano wa Eliya ulikuwa sawa na wa Yohana.

Na nabii maisha yake yote ni maisha ya ujumbe na ndiyo maana walivaa mavazi ya aina ile. Eliya alinyanyuliwa kuwa nabii katika kipindi kigumu sana. Kipindi ambacho Yezebel alikuwa amefundisha watu wa nyumba ya mfalme kumwabudu baali na manabii wa baali walikuwa wakila chakula katika meza ya mfalme.

Katika Israel walipokuwa wakiomboleza wakiwa katika majonzi walikuwa wakivaa mavazi ya namna hiyo. Na kufuatana na vazi na alikuwa ni Nabii wa moto na ndiyo maana Yohana mbatizaji alileta ujumbe wa moto.

2 Wafalme 18:21-24 Na hapa tunaona Eliya akimwelezea Mungu kwamba “Mungu anayejibu kwa moto na awe Mungu” Nguvu iliyomo katika moto ni kali kwa hiyo kitu chochote kilichoungua hakiwi na sura ile ya zamani kinabadirika. Hivyo moto wa Roho Mtakatifu unakuachia alama ya kudumu katika maisha yako.

Moto wa Roho Mtakatifu ni kizingiti kati ya Mungu na uovu tunatakiwa kuondoka katika maisha ya ukristo rejareja na kuingia katika maisha ambayo Mungu anayataka tuishi. Katika kutakasika Mungu anajidhihirisha kwetu, na hapa Mungu anatafuta watu watakaokuwa kiwango chake!! Pia kumbuka kuwa Mungu hawezi kubadirika kiwango chake bali wewe ndiwe unayetakiwa kubadirika.

Katika Biblia moto unazungumzia juu ya Utakatifu au usafi. Moto unasafisha uchafu wote vitu vyote katika agano la kale vilivyotumika mbele za Mungu (yaani vikombe na mabakuli) Mungu alitaka view vya Dhahabu safi. Na tunaona kuwa Dhahabu safi hupatikana baada ya kupitishwa kwenye moto. Dhahabu safi inamaanisha utukufu wa Mungu.

Malaki 3: 1-6 Hapa tunaona malaki akitoa unabii juu ya Bwana ambaye yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha na ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo, anasema atakapo kuja yeye huyo ambaye ni moto atatawala na kuharibu kila kitu kichafu. Hakuna namna ambayo tutaweza kuendelea mbele isipokuwa tumekabiliana na mto wa moto. Mungu anapotaka kutunza uhalisi ni lazima atumie moto. Nabii Isaya naye alikusudiwa na Mungu ili awe kiwango cha Mungu kwa ajili ya wengine, hivyo Mungu alimgusa na kumtakasa.

Bwana anataka kusafisha uwanda wake, na uwanda wake ni Kanisa, kwa hiyo lazima ibaki mbegu iliyosafi katika Kanisa.

Kila aina yoyote ya ubinafsi, kiburi, tamaa, hila na uchafu wowote vinatakiwa kupambanishwa na moto wa Roho Mtakatifu. Ukipokea ubatizo wa moto huwezi kuishi katika uasi na uchafu. Baada ya kupokea moto wa Roho Mtakatifu ukijichanganya na kuishi katika maisha ya dhambiHUTAFANIKIWA, moto wa Bwana utakufuatilia.

Katika Kanisa Ibada ya Sanamu imeshamiri.

Ibada ya Sanamu ni nini?;

Ni kile kitu chochote kinachochukua nafasi ya Mungu katika maisha ya mtu /yako. Mala zote Mungu alipotaka kufunga agano na watu wake aliwakumbusha laana zote walizopata pale walipovunja agano lake.

Mungu ni moto ulao, moto unakaa juu ya uwepo wake Roho Mtakatifu na moto wake unaposhuka kila kichafu kinaondolewa. Mungu anatunza kitu halisi kwa kushusha moto wa Roho Mtakatifu. Uwepo wa Mungu ni moto kwa hiyo unaposhuka lazima utakula kila kitu kichafu. Mungu ana mengi zaidi aliyokusudia katika maisha yetu. Mpango wa Mungu katika maisha yetu ni mkubwa sana hatujafikia hata nusu ya mpango wa Mungu katika maisha yetu kwa hiyo hatutakiwi kuridhika. Ukiona umeingiliwa na roho ya kuridhika jua kwamba roho ya kiburi tayari imekwisha kuingilia. Vitu vyovyote vinavyoweza kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yetu ni “Kinyago” sanamu. Mungu hatabebana na vitu vyovyote visivyo sawa katika maisha yetu.

Tunahitaji kupona na kubadilika ili Mungu atusahihishe. Roho yuko tayari kuteketeza kila kitu kisichofaa ndani yetu. Baada ya ubatizo wa Roho Mtakatifu huwezi kustawi katika maisha ya kumwasi Mungu. Ukifanya hivyo mambo yako hayatakuendea vyema katika kumuasi Mungu.

1Yohana 5: 18 Tofauti iliyopo kati ya mtu wa Mungu na asiye wa Mungu ni kwamba mtu wa Mungu hata ikitokea akakosea kwanza anasikitika na anafanya jitihada za kushinda ile dhambi (kuindoa).

Mtu anayeendelea kufurahia dhambi atakuwa anakabiliwa na moto wa Mungu.

Pepeto liko mkononi mwa Bwana. Ili tusimame kama jamii ya kinabii ni lazima tusikie joto la Roho Mtakatifu kwanza. Hakuna sababu ya kuwaonya watu wengine ili watubu kabla hatujalipata joto la Roho Mtakatifu sisi wenyewe.

Lazima tujipange sawasawa na Bwana. Lakini hakuna namna tunayoweza kujipanga na Mungu mpaka tutakapo ruhusu moto wa Roho Mtakatifu ututakase.

Mambo mengi tunayoona ya kawaida ambayo hayako katika mpango wa Mungu sio ya kawaida na hii ni kwa sababu ya hali ya ubaridi ulio katika Kanisa lakini ukiruhusu moto wa Bwana mambo yote maovu yataondoka.

Petro alikuwa na moto wa Roho Mtakatifu ndio maana aligundua kile alichofanya Anania na mkewe.

Ujazo wa Roho Mtakatifu unapokuja katika maisha yetu kuna mambo ambayo hatakubaliana nayo.

Tunapotaka kwenda mbele na kutembea vizuri na Mungu katika maisha yetu tunatakiwa tuwe watu ambao tutaweka kando kila namna ya uchafu. Ubatizo wa moto ni ubatizo ambao unashughulikia dhambi katika maisha yetu.

Mungu atusaidie kutembea katika utakatifu wote na kukubali kubatizwa na moto wa Roho Mtakatifu.

 

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU