YESU ALIDHIHIRISHWA ILI KUHARIBU KAZI ZA SHETANI.

1.Kazi za Mungu ni zipi na kazi za shetani ni zipi?

Tangu kale watu walijua kazi za Mungu zina msaada kwa mwanadamu Zaburi 78:4, 12-15,26; 92:4, 13-15.

Yesu alipokuja alikuwa akifanya kazi za Baba yake . Kisa cha uponyaji katika birika Yohana 5: 17, 20, 36; Yohana 10:27. Hivyo tunajua kazi alizotenda Bwana Yesu zilikuwa njema Matendo 10:38

Kazi za shetani alizokuja kuharibu Bwana Yesu ni zipi? Tukitazama yale aliyofanya Bwana tunagundua kazi za ibilisi ni pamoja na magonjwa. Luka 13:16. Tazama Yohana 10:10

2.Yesu alichukua mwili ili aharibu kazi za shetani.

Shida zilizokuwa katika mwili wa binadamu hakuna anayeweza kuzimaliza isipokuwa kwa kung’oa chanzo chake. Ndiyo maana ilibidi Yesu atoke mbinguni, akachukua mwili wa kibinadamu ili akamate mhalifu katika maficho yake. Waebrania 2:14

Dhambi na magonjwa vyote vilitokea kona moja na vinampeleka mwanadamu katika uharibifu. MAUTI MAUTI!!!

3.Damu yake ilipomwagika

Biblia utufundisha uzima umo katika damu. Walawi 17:11.

Kwa vile shetani ameleta mauti Yesu alimwaga damu pale msalabani ili uzima wa Mungu ufike duniani na kuwafikia wanadamu.

Damu ilipomwagika ushindi ulikuja kwako kwa uzima wa Mungu na ulimeza mauti. Ufunuo 12:11

4.Mabadilishano Kalvari.

Kazi ya ajabu ilifanyika pale Kalvari ni mabadilishano. Yesu akichukua shida zetu na kukabiliana na ugumu wake na kutupatia Baraka zake. Isaya 53:4-5; Mathayo 8:17; 1 Pet 2:24.

Yesu anaonekana katika sura ya jenerali aliyeshinda vita. Wakolosai 2:13-15

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU