IJUE VITA YAKO(3)

MAUNGAMO KINYUME NA UKWELI ANAOSIMAMA NAO KRISTO KAMA WAKILI

Waebrania 4:

14 Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.........

23 Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumba–yumba, kwa maana Yeye aliyeahidi ni mwaminifu.

Watu wengi wanaipoteza imani yao kwa kukiri mambo kinyume na neno la Mungu, kinyume na ukweli. Kukiri ni kutangaza msimamo, ni kuweka wazi kile unachosimamia. Sasa unapokiri kimyume na kile anachosimamia Bwana Yesu kama kuhani na wakili wako, hapo unavunja uwezo wa Bwana Yesu wa kukusaidia. Zaburi 78:41

Maneno yako ndiyo chombo kinachobeba imani yako. Imani imebebwa ndani ya maungamo yako. Ukidumu kusema yale anayoyaweza shetani juu yako, vile anavyokuonea na kukuzuia, huwezi kuona ushindi. Mbona usiseme jinsi Mungu anavyoweza na alivyo na nguvu katika maisha yako?

Maungamo yako huweka wazi msimamo wako wa kiimani kwa kuthibitisha na kushuhudia yafuatayo:-

1. Yale ambayo Mungu ametufanyia kwa njia ya Kristo katika mpango wake wa wokovu.

2. Jinsi tulivyo mbele ya Mungu katika Kristo.

3. Mambo Mungu kupitia Neno lake, Roho mtakatifu ametutendea tulipozaliwa mara ya pili na katika kujazwa na Roho Mtakatifu.

4. Kile anachofanya Yesu mkono wa kuume wa Baba anaishi daima akituombea.

5. Yale Mungu anayoweza kutenda kupitia sisi au yale neno la Mungu linachoweza kutenda tunapolitangaza.

Mungu siku zote hutenda kazi kupitia mwamini kulithibitisha neno lake.

Marko 16:

20 Kisha wanafunzi Wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo. Amen.

Maungamo yanashuhudia juu ya ukweli unao ujua. Unakiri juu ya haki zako na mafao mbali mbali uliyo nayo katika Kristo,aAmbayo tayari unayamiliki kutokana na kazi ya Kristo pale msalabani?.

Biblia huonyesha watu hupata kile wanacho kiamini toka katika neno la Mungu pale wanapougama kwa vinywa vyao

Warumi 10:

10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo uhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.

Hapa mtume Paulo anaongelea juu ya kupata wokovu, anasema mtu hukiri kuwa ameokoka ndipo hupata wokovu. Lakini huu ni ukweli hata kuhusiana na mambo mengine unayohitaji toka kwa Mungu. Kwa mfano kwa kinywa mtu hukiri uponyaji wake kwa njia ya mapigo ya Kristo pale msalabani hata kupata uponyaji. N.k

Kama huna furaha na yale uliyo nayo leo basi badili maungamo yako. Maana umepata yale uliyo kuwa ukiyakiri kwa kinywa chako.

Kwa mfano Israel wa zamani walipata kile walichokiri masikioni pa Mungu.

Hesabu 14:

1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! Kwa nini BWANA anatuleta katika nchi hii ili

Wana wa Israel baada ya kusikia taarifa ya wapelelezi kumi wasiokuwa na imani tena na Mungu waliambukizwa kutokuamini. Kisha wakasema kwa vinywa vyao “bora tungefia katika jangwa hili” Na Mungu akawaambia mmetegwa kwa maneno ya vinywa vyenu. (Mithali 6:.. umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,)

Hivyo anawajibu Israel kulingana na maungamo yao ..

Hesabu 14:

26 BWANA akamwambia Mose na Aroni: 27‘‘Jumuiya hii ovu itanung’unika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonung’unika. 28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asema BWANA, nitawafanyia vitu vile vile nilivyosikia mkisema: 29 Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na ambaye amenung’unika dhidi yangu miili yenu itaanguka katika jangwa hili. 30 Hakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu,

Unajua mauti na uzima vimewekwa katika uwezo wa ulimi wako. (Mithali 18: 21 Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.)

Watu wengi wanapoteza Baraka na miujiza yao kwa kushikilia maungamo yanayopingana na Neno la Mungu baada ya maombi na katika maisha kwa ujumla. Yesu ni kuhani wetu mkuu anashikilia maungamo mema kwa ajili yetu, nasi tunapaswa kutunza msimamo huo huo alio nao BwanaYesu kwa ajili yetu mbele za Baba. Kama Yesu anasema dhambi zao zimesamehewa kwa mauti yangu basi nasi tukiri “Nimesamehewa dhambi zote kwa mauti ya Bwana wangu Yesu.” Kama Yesu anasema nimewapatia ushindi dhidi ya ibilisi na jeshi ovu la shetani basi tukiri kuwa “mimi ni zaidi ya mshindi kwa Yeye aliyenipenda…”Kama Yesu anasema nimechukua udhaifu wao kwa mapigo niliyopata pale msalabani basi sisi tukiri “na kwa mapigo ya Bwana Yesu mimi niliponywa na hivyo ni mzima.”

Basi ndugu ili kushinda vita jihadhali usishindane na neno la Mungu katika kukiri kwako bali ukubaliane nalo. Amen.

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU