KIWANGO CHA MUNGU.

Somo hili la kiwango cha Mungu ni mfululizo wa masomo mengine mengi yanayofanana na kurandana nalo. Na katika utangulizi au mwanzo wa somo hili tutaangalia juu.

SEHEMU 1

KUTUNZA KIWANGO CHA MUNGU KATIKA MAISHA YETU

Tuanze kujifunza somo hili kwa kuangalia Malaki 3:6 katika mistari hii ya malaki tunaona kuwa Mungu habadiliki ni yeye yule jana leo na hata milele. Hivyo bali kiwango chake lazima kiwe kile kile jana leo na hata milele.

Kiwango tunaweza kukilinganisha na bendera kuwa bendera inaweza kuwa inatangaza jambo Fulani linaloeleweka kadhalika na kiwango. Hivyo katika masha yetu ili kutunza kiwango cha Mungu hatuna budi kuishi maisha ya haki.

SEHEMU 2

KUTUNZA KIWANGO CHA MUNGU KATIKA UTAWALA NA SIASA

Tuendelee kuangalia somo hili la kiwango cha Mungu hata ndani ya utawala na siasa. Na kwa kuanza basi tuangalie mistari ifuatayo: 2Nyakati 26: 1-5, 16-19

Katika mistari hiyo hapo juu tunasoma juu ya mfalme uzia, aliyefanywa mfalme akiwa na umri mdogo sana baada ya kifo babaye. Mfalme huyu alimtafuta Bwana sana na kutaka kujua mapenzi ya Mungu kwa kufanya hivyo Mungu alimfanikisha sana. Hali hiyo ilimfanya mfalme huyu kuwa na kiburi machoni pa Bwana na hata kufanya kazi asizotakiwa kufanya kama kufukiza uvumba.

Mfalme huyu alikataa hata kuwatii makuhani ambao ndio waliwekwa wakfu kwa ajili ya kufukiza uvumba. Adhabu yake ilikuwa ni kupigwa ukoma tena mbele ya wale makuhani. Mfalme huyu ni mfano wa wafalme au waliopewa madaraka kisiasa wakaonywa na kuadhibiwa kwa kutotunza kiwango cha Mungu katika utawala wao na kisiasa.

Sasa tuangalie tena katika Mithali 8:15 Katika mistari hii ya mithali tunaona kuwa msaaada wa wafalme upo kwa Bwana. Pia na wahukumu kwa msaada wake wanahukumu kwa haki. Hili ndilo suala la kuwanusuru viongozi na watawala. Mungu anaendelea kututahadhalisha juu ya kutotii na kutokutunza kiwango chake katika utawala na siasa.

Daniel 14 :32 Pia yeye ndiye muweza wa yote anayeweza hata kuwaondoa na kuwaweka viongozi.

Daniel 2 :21. Katika suala zima la kiutawala na kisiasa jambo muhimu la kuangalia ni vipi unatembea na Mungu wako na kipimo cha kuangalia uko vipi kiroho ni pale mambo yako ya kimwili yanapoanza kuenda kombo. Hapo ndipo utakapotakiwa kujipeleleza zaidi kiroho. Na utakapo-gundua kosa mara moja ukatengeneza ndipo hata utawala wako utakapokwenda sawasawa. 2Wafalme 21 :1-6,16. Hivyo masuala ya siasa na ya kiroho ni pande mbili za shilingi.

SEHEMU YA 3

KIWANGO CHA MUNGU CHA KINABII KATIKA MAISHA YETU

Sasa hebu tuangalie kiwango cha Mungu cha kinabii katika maisha yetu Luka 13 :31-35 Katika mistari hii hapo juu tunaona juu ya Yerusalemu awauwaye manabii. UNABII Ni ujumbe unaotumwa na Mungu kwa kusudi maalumu kati ya watu wake. Unabii unapotoka unalenga kurekebisha kuonya, kukosoa na kukemea.

Sasa tuangalie tunaitikia vipi :

CHANGAMOTO YA KINABII

Katika somo hili tunakusudia kuangalia kitu cha kufanya unapoletewa unabii au neno la Bwana. Katika jamii ya kinabii ni lazima pawepo na watu wanaopenda kutunza kiwango cha Mungu na wanaopenda kweli na kuishi katika hiyo.

MATATIZO KATIKA KUPOKEA NENO LA KINABII.

Kuna baadhi ya matatizo yanayofanya neno la kinabii kupokelewa tofauti na lengo au kusudi lake. Baadhi ya matatizo hayo ni kama

I) Kukubaliana na kila kinacholetwa mbele zetu kama neno toka kwa Bwana na hivyo kuangukia katika mikono ya manabii wa uongo.

II) Kuishi na hofu ya kudanganywa na manabii wa uongo na hivyo kukataa hata neno ambalo lingeweza kutusaidia. (yaani neno halisi la kinabii).

III) Kushindwa kulipima neno la Bwana na hivyo kuchanganyikiwa na kuitikia vibaya ujumbe wa kinabii. Hivyo ili kukabiliana na shida namba (I) na II hatuna budi kujua jinsi ya kupima unabii au ujumbe wa neno la Mungu ili tufahamu ikiwa ni wa kwake au la.

SULUHISHO.

Kabla ya kuchukua hatua yoyote unapoletewa neno la kinabii au ujumbe wa neno la Mungu ni kulipima neno hilo.

1Yohana 4 :1 Wapenzi msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wengi wa uongo wengi wametoka duniani na tena, ujaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema.

1Thesalonike 5 : 21 Hivyo tusipolipima neno hilo tunafanya dhambi, maana dhambi ni uasi na uasi ni kutotii au kukiuka maelekezo

JINSI YA KUPIMA NENO/ UNABII

Ili tupime neno tunahitaji kipimo na kipimo kinategemea kiwango cha kibiblia maana unabii hautaletwa popote na kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na roho wa Bwana 2Petro 1.21.

Mtume Paulo akisisitiza kwa watu wa korintho kupima kwanza neno la kinabii na sasa tuangalie vipimo vya kipimia neno linalotoka kwa Bwana.

Je unabii unapatana na maandiko au neno la biblia ?

Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na roho mtakatifu. 2Petro 1 :21

Neno linalotujia lipatane na yale yaliyokwisha kuandikwa katika Biblia. Mfano kuna watu walipata unabii kwa tarehe fulani wapande mlima na kukutana na Bwana Yesu na kuwa ndio siku ya unyakuo. Lakini tayari Biblia inaeleza wazi kuwa Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye hata malaika walio mbinguni wala mwana, ila Baba peke yake Mathayo 24 :36

Je unabii unaimarisha agano lake na Mungu. Au watupeleka mbali na Mungu ?

Kukizuka katikati yako unabii akikutolea ishara au ajabu ikatukia akisema tuitumikie hiyo wewe usiyasikilize maneno ya nabii yule na yule nabii au yule mwotaji wa ndoto na wewe... Kum. 13 :1-5

Sisi tuna agano la kumwishia Bwana na kutembea pamoja naye. Hivyo hakuna ujumbe toka kwa Bwana. Unaweza kutuhimiza au kusababisha tuvunje agano naye na kuiandama dunia. Hivyo hakuna Mungu wa kuongea jambo kisha akajikanusha.

Je lile neno au unabii linatupa hiari ya kuamua au linatulazimisha kwa vitisho ?

Basi Bwana ndiye roho walakini alipo roho wa Bwana ndipo penye uhuru 2Korintho 3 :17.

Je lile neno au unabii linatupa hiari ya kuamua au linatulazimisha kwa vitisho ?

Basi Bwana ndiye roho walakini alipo roho wa Bwana ndipo penye uhuru 2Korintho 3 :17. Pamoja na faida kubwa iliyopo ndani ya wokovu bado Mungu amewaacha wanadamu kuamua au kumpokea Bwana Yesu awaokoe au kumkataa, wakaenda motoni. Hata katika mambo mengine Mungu anayoyafanya na sisi anatuacha tuchague kumtii yeye anachosema au la, hatulazimishi. Mungu anachofanya katika maisha yetu hukiweka katika mioyo yetu ili tukifanye kwa hiari yetu tukihimizwa tokea ndani.Kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu ili kutaka kwenu na kutenda kwenu na kulitimiza kusudi lake jema Wafilipi 2 :13

Ukiona mtu analeta neno na anakulazimisha kutii weka alama ya kuuliza. Au ukiona mtu analeta ujumbe katika hali ya utisho na kudhoofisha nafsi yako ya kuamua kutii au la basi jua hapo kuna tatizo.

Je neno lililosemwa linatimia ?

Ikiwa Bwana amesema jambo atalitimiza yeye hawezi kusema uongo. Ikiwa neno lile lina masharti basi masharti yake yakitimizwa litatendeka kama Bwana alivyosema.

Nawe ukisema moyoni mwako tutajuaje neno alilolisema Bwana ? atakaponena nabii kwa jina la Bwana lisifuate jambo like wala kutimia hilo ndilo neno alilolinena Bwana .... Kumb. 18 :20-21

Ukiona mtu aliyeleta neno wakati fulani anakupa maelezo ya kutetea kwanini jambo alilisema na lile neno halikutimia jua halikutoka kwa Bwana. Maana Bwana hahitaji kutetewa na mtu.

Je neno au unabii unapeleka utukufu wapi ?

Ikiwa linakujia neno ambalo utukufu na heshima haiendi kwa Yesu bali inaenda kwa mtu kikundi au dhehebu uwe mwangalifu na neno hilo. Ukiona unapata neno la kuinua mtakatifu hakuhusika katika shughuli hiyo. Yesu alipoeleza wanafunzi juu ya ujio wa roho katika Yohana 16 :14 Anasema yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari kwa hiyo nawaarifu ya kwamba hakuna mtu aliye katika roho wa Mungu kusema Yesu amelaaniwa wala hawezi mtu kusema Yesu ni Bwana isipokuwa katika roho mtakatifu

1Wakorintho 12.3 Ukiona mtu anakuletea neno huku akitaka umaarufu na ubora alio nao jua mtu huyo anajitafutia utukufu. Wengi wa hao hupenda kutumia unabii kuwafanya watu wamwandame na kumsikiliza. Watu wa jinsi hii ni hatari katika mwili wa kristo.

Je maisha ya mtu yana matunda ya tabia njema ya kikristo ?

Bwana yesu akitaadharisha juu ya manabii wa uongo alisema mtawatambua kwa matunda yao. Mathayo 7 :15-16. ikiwa mtu anayeleta neno la Mungu kwake anaishi katika dhambi na hafanyi jitihada yoyote kuishinda na kuitubu usikubaliane na neno lake. Maana kama kweli anasikia toka kwa Mungu angesikia neno la Mungu kwa ajili ya maisha yake na hitaji lake la kutubu.

Ushuhuda wako wa ndani unasemaje ?

Roho mwenyewe ushuhudia pamoja na roho zetu Warumi 8 :16 na tena ; Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu ndiyo mliyoitiwa.... Wakolosai 3 :15

Pamoja na mambo mengine yote jua kuwa Roho mtakatifu anawasiliana nawe kupitia katika roho yako ikiwa umezaliwa mara ya pili. Neno la Mungu hutufundisha kuwa roho ya mwanadamu ni taa ya Mungu na pia kwa vile tumezaliwa upya katika roho zetu inakuwa rahisi Roho mtakatifu kuleta ujumbe katika roho zetu kama kuna amani moyoni na ujumbe basi usiutelekeze na kama huna amani nao chukua muda uombe ili kujua kwa nini huna amani nao.

Haya ni kati ya mambo ya kukusaidia kupima. Kuna mengine zaidi ambayo tutayaangalia katika masomo yanayofuata lakini haya tu ukiyatumia tayari yatakunusuru na ajali nyingi za kiroho.

JE UNAIPONYA NAFSI YAKO AU UNAIANGAMIZA ?

LUKA 9 :23-25 "Akawaambia wote, mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake kila siku anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza na mtu atakaeiangamiza nafsi yake kuwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote kama akijiangamiza au kujipoteza mwenyewe?"

Maneno haya aliyasema Yesu mwenyewe na kufaa kama njia kwa mtu yeyote aliye tayari kumfuata ajitwike msalaba wake kila siku na amfuate. Haya ni masharti ya Yesu kabla ya kuondoka. Inaweza kukufikirisha kuwa unaiponya nafsi yako kumbe unaiangamiza.

Bwana Yesu anasema kuwa anayetaka kumfuata ajikane. Hapa kunaweza kuwa kumkana mwenyewe maana ile ya kwanza inaweza kufanana kabisa na ile ya Yuda Iskariote ya kumkana Bwana Yesu. Yuda alijikana mwenyewe kumjua Bwana Yesu. Lakini maana ya pili ni ile ya kukataa mambo unayoyapenda wewe mwenyewe kuyakataa kwa ajili ya Bwana yaani kuacha vyote. Unasikiliza Bwana wako anasemaje hata kwa vitu vyako mwenyewe. Kwa mfano una gari lako lakini hulitumii upendavyo bali Bwana apendavyo. Bado unaweza kuwa na pesa ni zako mwenyewe.

Tunaweza kupata mfano mzuri kutoka kwa mtumwa na Bwana wake. Mtumwa sharti asikilize Bwana wake anasemaje, akiona kama muda huu autumie kulala Bwana wake anasema kachote maji na anakubali kwa kuwa ni Bwana wake amesema.

Yesu mwenyewe ni kielelezo cha haya yote hata yale aliyoyataka kuyafanya au jinsi alivyopenda mwenyewe hakufanya ila alimwacha Bwana yaani Baba yake na mara zote alikiri kuwa mapenzi yako yatimizwe.

Wafilipi 2 :5-8 Katika mistari hii tunaona kuwa Yesu mwenyewe alijifanya si kitu akanyenyekea hata mauti ya msalaba. Ndio maana anasema kuwa yeye anayetaka kumfuata na ajitwike msalaba wake kila siku amfuate. Msalaba hauna maana ya ugonjwa wa muda mrefu kama wengi walivyozoea kusema.

Msalaba una maana kuomba ni ishara ya maumivu.

Kati ya watu tunaowaona kuwa ndio kielelezo cha kubeba msalaba katika Biblia ni Yusuph, Daniel, mwanamke mjane wa serepta, watu hawa walijikana walijitwika msalaba wao wenyewe.

Mungu anasema kuwa kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu na kupoteza nafsi yake mwenyewe. Hakika hakuna faida yoyote.

JE UNAIPONYA NAFSI YAKO AU UNAIANGAMIZA

Luka 9 :23-25 Yesu alisema maneno hayo alipokuwa anakaribia kuja msalabani. Alisema kama mtu anataka kumfuata yako masharti ni lazima aikane nafsi yake na ajitwike msalaba wake kila siku amfuate

Masharti ya ufuasi ni : Masharti ya ufuasi ni :

-Kukana ni kukataa hadharani

- Kukana ni kuukataa ubinafsi

- Kukana ni kutoa maisha yako na kumpa Yesu ili ayatawale.

- Kukana ni ile hali ya kushinda mapenzi yako ya binafsi na kumwachia Mungu aweze kutawala.

- Kukana ni kukubali kabisa kutawaliwa na mapenzi ya Bwana.

- Kukana ni kukubali kuachilia ndoto zako mipango na hali yako na kumwachia Bwana atawale.

Yesu kristo ndiye kielelezo cha kujikana Filipi 2 :5-8

2. Lazima kujitwika msalaba kila siku na kumfuata yesu msalaba ni alama ya mateso, aibu kukataliwa na hata kudharauliwa.

Yeye aliyetutangulia ni kama alionyesha ni njia ipi tutakayopitia yaani njia ya mateso. Luka 9 :23.

Watu walio tayari kumfuata Yesu kubeba msalaba kitu chochote hakiwatengi na Bwana na wako tayari kufanya chochote kile Bwana anachowaagiza kufanya.

Watu wanaoziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Bwana hao ndio Bwana anaowataka.

Kama hujamwachia Yesu maisha yako ili ayatawale unakuwa unaamua kama unavyotaka mwenyewe.

Kanuni ya Yesu ni kama unataka kumfuata ni lazima ujikane mwenyewe ujue kuwa wewe ni mali ya Bwana.

Lazima tujue kuwa Mungu anatufahamu kabisa na anatukumbuka.

Hebu tujikane wenyewe, tukatae njia zetu na tukubali Bwana atuendeshe mwenyewe.

Tunatakiwa kumtii Bwana na kufuata vile anavyotaka.

Luka 17 : 32-33 Mke wa Lutu alipoamua kujiponya alijiangamiza.

Galatia 6 :12-14 Mtume Paulo alisema haoni fahari kuwa kitu kingine chochote bali anaona fahari juu ya Bwana.

Angalizo: Hebu tuangalie maisha yetu wenyewe je tunajenga wapi ?

Anayefikiri anaiponya nafsi yake anaiangamiza lakini anayeipoteza kwa ajili ya Bwana anaiponya.

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU