KUONA NYUMA YA MLIMA

Mlima unaweza kwa hali ya kawaida kutafsriwa kama kizuizi kikwazo au kipingamizi. Kama ni safari maana yake ni kwamba ukikutana na mlima umekutana na kizuizi cha safari yako.

Katika Biblia ni tofauti, kwani si milima yote inasimama kama vizuizi bali milima mingine ni baraka au neno mlima lina maana ya ufalme wa milele, watawala na wakuu.

Tunapozungumza juu ya mlima hatuna budi kuzingatia kuwa kuna hatari pande zote mbili: mfano Musa aliwaambia wana wa Israel kuwa kuna hatari jwangwani yaani na hata kanaani watu wajue hilo na pindi wafikapo tu nchi ya ahadi, nchi yenye maziwa na asali wasimsahau Mungu na kusema kuwa tumeyapata haya yote kwa juhudi zetu.

Kwa hiyo tunaweza kuona kuwa kuna hatari katika mafanikio na pasipo mafanikio.

Zaburi 121. Katika Zaburi hii muimba Zaburi anasema kuwa atainua macho yake aitazame milima (Au kwa maana nyingine macho yake yatatazama nyuma ya mlima) msaada wake utatoka kwa Bwana, ambaye anaweza kufanya yote. Milima aitazama kama magumu ya maisha lakini nyuma ya milima hiyo anamuona Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, hivyo anapata tumaini la maisha yake.

Hivyo basi hali hii ina muandaa muamini kuona nyuma ya mlima na kuona vilivyopo nyuma ya mlima. Ni rahisi kuona shida taabu na ukabaki tu ukiitazama hiyo milima na usimuone Mungu ambaye yuko nyuma ya milima hiyo. Vile vile ni rahisi kumwangalia na kumtegemea mtu ambaye anaweza kuwa msaada kwako pasipo kuangalia nyuma ya mtu kuwa kuna Mungu mwenyewe ndiye anayefanya hayo yote. Mfano kuna mzazi ambaye ana watoto 3 mmoja yuko Ulaya mwingine yuko Amerika na mwingine anaishi naye, lakini tumaini lake lote liko kwa wanawe hao kiasi kwamba anaweza kutembea kwa kujivuna kwamba dunia yote ni ya kwake bila kumwangalia aliye nyuma ya watoto wake anaowaona kama nguzo zake kuwa ni Mungu.

Asipomuona Mungu nyuma ya milima anajipa matumaini ya uongo. Tunahitaji kumuona Mungu nyuma ya vitu vyote. Msaada wa muimba Zaburi hautoki kwa vitu unatoka kwa Bwana.

Tunapoendelea mbele na somo hili tunajifunza kuona kutoka kwa Bwana tunaweza kufikiri au kuona kuwa changamoto inatoka iwapo una mchumba au la, una mtoto au la. Maana unaweza kupata shida kwa kuwa na mchumba, vilevile unaweza kutokuwa naye ukapata shida. Unakuwa na shida ya kutokuwa na mtoto vilevile ukampata ukawa na shida.

Musa anawaambia wana wa Israel kuwa huko mwendako katika nchi ya ahadi baada ya kuvuka Yordani wasije wakamsahau Mungu na kusema kuwa haya yote tumeyapata kwa juhudi zetu wenyewe. Walichotakiwa kufanya ni kumwangalia Mungu nyuma ya hayo mema yote Kumb. 8:24

Sio wote wanaosafiri katika safari moja mnaenda sehemu moja. Hivyo basi tunapokwenda mbele ni lazima tuwe na mapinduzi ya Habakuki. Habakuki 1:1-4 Mungu anawatayarisha watu wasiomjua ili kuwatumia kuwaadhibu watu wake. Yaani Wakaldayo. Habakuki anamwambia Mungu kuwa mbona watu wake wanafanya uovu waziwazi. Hivyo Mungu anafanya mpango wa kuwaadhibu watu hawa. Mungu anamwambia Habakuki kuwa anamwandalia watu wasiomjua (Wakoldayo). katika hali ya namna hiyo Habakuki anamlalamikia Mungu kuwa inakuwaje awatumie watu hawa wasiomjua hivyo Mungu anasema kuwa Habakuki asiwe na wasiwasi pamoja na kasi na nguvu za Wakoldayo mwenye haki wa Mungu ataishi kwa Imani.

Tuzungumze au tuangalie kidogo juu ya hili. Zipo haki za namna mbili yaani haki ya kuhesabiwa na haki ya kudhihilishwa wewe mwenyewe. Kwa mfano unapokuwa mahala ukaona haki inadhulumiwa na mtu anaibiwa waziwazi wewe ukakaa kimya na kudai kuwa wewe umehesabiwa haki bure unajidanganya.

2Kor. 11.3 Hivyo inaposemekana kwamba mwenye haki wa Mungu ataishi kwa Imani udanganyifu na hila hauendani na mtu mwenye haki. Habakuki 2:7-8 Tunatakiwa tunapoomba tuombe sawa sawa na ahadi za Mungu. Tumwangalie Mungu aliye nyuma ya shida au jaribu tulilo nalo na anasemaje juu ya hilo.

Kumb. 43: 21 Tumkumbushe Mungu juu ya yale aliyosema. Habakuki 3:18 Siri ya mafanikio ya Habakuki kulingana na uamuzi wa Wakaldayo ilikuwa ni kumwangalia Mungu aliyosema nyuma ya Wakaldayo. Ufumbuzi tunaweza kusema kuwa Habakuki aliona nyuma ya mlima

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU