UPANDAJI MAKANISA VIJIJINI.

“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20 nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen. Mathayo 20:18-19

Katika kutimiza agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo huduma ya Rhema Outreach Ministries imeanza mpango wa kupanda makanisa vijijini. Mpango huu unatumia njia ile Bwana yesu aliyoagiza ifuatwe. Yaani watu wenye wito na mzigo wa kumtumikia Mungu katika ngazi ya kulea watu kiroho wanachukuliwa.

Hatua ya kwanza wanapewa mafunzo ya awali ya namna ya kwenda katika eneo jipya lisilo na kanisa na kuanzisha kanisa yeye mwenyewe. Kisha mchungaji huyu anapewa mafunzo ya masomo ya mwanzo ya uanafunzi. Mchungaji anakwenda na kuanza kuyafundisha kwa waamini hawa wapya. Wakati huo huo mchungaji huyu anaanza kufundishwa masomo mbali mbali ya biblia kila mwezi masaa 20 kwa kutumia kozi inayoitwa Omega. Kozi hii imetayarishwa kwa ushirikiano na wadau mbali mbali wa mafunzo ya Biblia kwa watumishi. Wakati anaendelea kujifunza na kulifundisha kanisa lake (wale waamini wapya) akiwapa yale masomo ya uanafunzi, anatafuta watu wengine wawili anaowashirikisha yale masomo yake ya kichungaji anayojifunza yeye. Wale watu wawili wanachukua hatua ya kuanzisha kanisa kama yeye alivyofanya.

“2 Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vile vile.” 1 Timetheo 2:2

Makanisa haya mapya mawili yanaendelea kulelewa katika mikono ya mchungaji wa kwanza hadi yakifikia hatua ya kuweza kujiendesha yenyewe jambo ambalo ndilo lengo kuu.

Mpango huu wa kusisimua tayari umeanza na tumewatuma wachungaji wa kwanza. Tunayo makanisa mapya 15 ya huduma ya Rhema ambayo ni:

1. BWENDE- BUGABO

2. RWINA – BUGABO

3. IBOSA – BUGABO

4. IHUNGO- BUGABO

5. BUNENA MWALONI-BUKOBA

6. KAHORORO- BUKOBA

7. IJUGANYONDO- KYAMTWARA

8. MARUKU

9. MAIGA

10. KIIZI- KANYANGEREKO

11. BITUNTU- BUJUGO

12. NSISHA-KANGABUSHARO

13. KYEGOROMOLA

14. KARWOSHE- KATOMA

15. BISHEKE- IHANGILO

Pia kuna kanisa la awali lililokuwa chini ya Rhema tangu awali la KEMONDO nalo linaendelea vizuri sana. Tayari kwa sasa kuna makanisa mawili ya kizazi cha pili yaliyozaliwa nayo ni:

1. BUHANGA- KIJIJI KATOJU

2. KISHOJU- MUBUNDA

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU

"1 Petro 1:22" Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo."