HUDUMA YA WATOTO

Ili kulitimiza agizo la Bwana Yesu katika kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu huduma ya watoto ilianzishwa. Yesu alisema “ waache watoto waje kwangu….” Wapo watu waliokuwa na mzigo na maono ya kuwafikisha watoto kwa Yesu. Huduma yetu imeamua kuchukua nafasi ya watu waliowaleta watoto kwa Yesu. Na kwa vile ni mapenzi ya Mungu kuwabariki na kuwahudumia basi kupitia huduma hii tunampa Bwana nafasi hiyo.

Huduma ya watoto ilianzishwa baada ya kuona wana fellowship wengi walio na watoto wanakuja nao ili na wao wapate mafundisho kila jumapili jioni wazazi wajapo kujifunza na hii ni baada ya kujua wazi kuwa watoto wa toka familia za wakristo ni kizazi nyeti kinachowindwa na adui shetani ili kuliaibisha kanisa na kuwakatisha moyo wazazi waliookoka ili warudi nyuma kiimani na kiroho.

Hivyo ni jambo la muhimu kuwafundisha watoto kumjua Bwana wetu Yesu Kristo na kuokoka. ( watoto pia wanahitaji kuokoka.) Na kwa sababu si rahisi watoto kuendana na mafunzo ya watu wazima, ilishauriwa ianzishwe huduma maalum ya kuwalea na kuwafundisha watoto wadogo kumjua Mungu kila wanapokuja na wazazi wao na hatimaye wakue wakimfuata yeye (Mithali 22:6)

Walimu katika kundi hili nyeti ni wana fellowship walio na wito wa kutunza na kufundisha watoto wadogo. Pia wamekuwa wakipata semina na mafunzo mbalimbali katika kumtumikia Mungu katika eneo la kuwafundisha watoto wadogo.

Watoto hujifunza kusifu, kuabudu, kuomba na ufundishwa neno la Mungu. Haya yote ufanywa katika muda ambao wazazi wao wanakuwa katika kujifunza pia. Baada ya kujifunza neno la Mungu, watoto upewa nafasi ya kucheza michezo mbalimbali kama mpira, Kuchora, wanasesere, kupiga kinanda na michezo mingi tu. Na yote haya ufanyika chini ya uangalizi wa wazazi walio na zamu ya kufanya shughuli hiyo wiki hiyo, maana baada ya mafunzo walimu wao uungana na wazazi wengine kujifunza neno la Mungu.

Kila wiki kuna zamu ya mtaa mmoja wazazi kucheza na watoto wote, hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanakuwa katika hali ya usalama na upendo katikati yao. Hii pia imesaidia sana kuwafanya na wazazi ambao ni wana fellowship kujifunza namna ya kulea watoto na jinsi ya kuwapa msaada kila panapokuwa na shida. Msaada mkubwa ikiwa ni kuwaombea na kuwashauri kupendana pale wanapotokea kwenda kinyume na maadili. Kwa mfano watoapo lugha chafu za matusi au wanapogombana.

Imekuwa ni ajabu sana kwamba watoto wengi wanaoendelea kukua katika huduma hii wanaonekana kuwa na maendeleo mazuri na wanaipenda sana.

Ni maono yetu kuwa tutakuwa na kizazi kilichofundishika kumheshimu Mungu katika siku zijazo na wazazi watakuwa wamefanikiwa kujifunza lakini pia na wana wao watakuwa wamefundishika kumuishia Mungu. Unaweza kutoa mchango wako katika huduma hii kwa kuiombea, kutupatia vitabu vizuri vya kikristo au vifaa vya watoto kuchezea ili tuwalee watoto wetu katika maadili mazuri ya kikristo. Unaweza kutuma mchango wako kwa anuani hii au kwa kujaza fomu hii hapa.

 

 

RUDI UKURASA WA KWANZA

RUDI MWANZO WA UKURASA HUU